وَيُنَجِّي ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْ بِمَفَازَتِهِمۡ لَا يَمَسُّهُمُ ٱلسُّوٓءُ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ ٦١
Wayunajjillāhul-ladhīnat-taqaw bimafāzatihim lā yamassuhumus-sū'u walā hum yahzanūn
Na Mwenyezi Mungu atawaokoa wenye kujikinga kwa ajili ya kufuzu kwao. Hapana uovu utao wagusa, wala hawatahuzunika. 61
Maelezo ya chini
61 Na Mwenyezi Mungu atawaokoa alio wajaalia ulinzi isiwapate adhabu ya Mwenyezi Mungu, kwa vile alivyo kwisha wajua kuwa wamefuzu, kwa walivyo ukhiari uwongofu kuliko upotofu. Na siku hii basi uovu hautawagusa, wala hawatahuzunika kwa kuzikosa neema walizo kuwa wakizitaraji.