وَأَنِيبُوٓاْ إِلَىٰ رَبِّكُمۡ وَأَسۡلِمُواْ لَهُۥ مِن قَبۡلِ أَن يَأۡتِيَكُمُ ٱلۡعَذَابُ ثُمَّ لَا تُنصَرُونَ ٥٤
Wa anībū ilā rabbikum wa aslimū lahū min qabli an ya'tiyakumul-'adhābu thumma lā tunsarūn
Na rejeeni kwa Mola wenu Mlezi, na silimuni kwake, kabla ya kukujieni adhabu. Kisha hapo hamtanusuriwa. 54
Maelezo ya chini
54 Enyi mlio jidhulumu nafsi zenu, rejeeni kwa Mwenye kuyamiliki mambo yenu yote, na Mlezi wenu. Na mfuateni Yeye kabla haijakujieni adhabu, tena hapo hapatakuwepo wa kukunusuruni na Mwenyezi Mungu na kukulindeni na adhabu yake.