Surat Az-Zumar, aya 36

39:36

أَلَيۡسَ ٱللَّهُ بِكَافٍ عَبۡدَهُۥۖ وَيُخَوِّفُونَكَ بِٱلَّذِينَ مِن دُونِهِۦۚ وَمَن يُضۡلِلِ ٱللَّهُ فَمَا لَهُۥ مِنۡ هَادٖ ٣٦

Alaysallāhu bikāfin 'abdahū wayukhawwifūnaka billadhīna min dūnihī waman yudlilillāhu famā lahū min hād

Je! Mwenyezi Mungu si wa kumtosheleza mja wake? Na ati wanakutishia kwa hao wenginewe wasio kuwa Yeye! Na aliye hukumiwa na Mwenyezi Mungu kupotea hana wa kumwongoa. 36

Maelezo ya chini

36 Mwenyezi Mungu, peke yake, ni Mwenye kuwatosheleza waja wake kwa kila lilio wakhusu. Na ati hao makafiri wa Kikureshi wanakutisha, ewe Muhammad, kwa miungu yao wanayo iomba badala ya Mwenyezi Mungu. Na hayo ni katika upotovu wao. Na mwenye kupotozwa na Mwenyezi Mungu, kwa kumjua kuwa huyo amekhiari upotovu kuliko uwongofu, basi hatakuwa na mwongozi wa kumwongoza.