Surat Az-Zukhruf, aya 9

43:9

وَلَئِن سَأَلۡتَهُم مَّنۡ خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ لَيَقُولُنَّ خَلَقَهُنَّ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡعَلِيمُ ٩

Wala'in sa'altahum man khalaqas-samāwāti wal-arda layaqūlunna khalaqahunnal-'azīzul-'alīm

Na ukiwauliza: Nani aliye ziumba mbingu na ardhi? Bila ya shaka watasema: Kaziumba Mwenye nguvu, Mjuzi! 9

Maelezo ya chini

9 Na ninaapa, ewe Mtume! Ukiwauliza makafiri nani aliye ziumba mbingu na ardhi? Bila ya shaka watasema kuyajibu hayo: Mwenyezi Mungu ndiye aliye ziumba, ambaye anasifika kwa hakika ya mambo kuwa ni Mwenye nguvu, na Mwenye Ujuzi ulio enea.