قُلۡ إِن كَانَ لِلرَّحۡمَٰنِ وَلَدٞ فَأَنَا۠ أَوَّلُ ٱلۡعَٰبِدِينَ ٨١
Qul in kāna lir-rahmāni waladun fa ana awwalul-'ābidīn
Sema: Ingeli kuwa Rahmani ana mwana, basi mimi ningeli kuwa wa kwanza kumuabudu. 81
Maelezo ya chini
81 Waambie hao washirikina: Ikithibitika kwa ushahidi kuwa kweli Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema ana mwana, basi mimi ningeli kuwa wa kwanza kumuabudu mwana huyo. Lakini hayo hayakuthibiti kwa hoja yoyote kwamba Rahmani ana mwana, kwa kuwa hayo ni kumfanya Mwenye nguvu awe hajiwezi, Mwenye kujitosha awe mhitaji. Na Yeye, Subhanahu, ametakasika na kila la upungufu kwa ukamilifu wake.