Surat Az-Zukhruf, aya 54

43:54

فَٱسۡتَخَفَّ قَوۡمَهُۥ فَأَطَاعُوهُۚ إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَوۡمٗا فَٰسِقِينَ ٥٤

Fastakhaffa qawmahū fa atā'ūhu innahum kānū qawman fāsiqīn

Basi aliwachezea watu wake, na wakamt'ii. Kwa hakika hao walikuwa watu wapotovu. 54

Maelezo ya chini

54 Firauni akawa anawachochea watu wake, na akawaathiri kwa udanganyifu huu, nao wakamt'ii katika upotovu wake. Kwani hao walikuwa watu walio kwisha toka kwenye Dini ya Mwenyezi Mungu Iliyo Nyooka.