Surat Az-Zukhruf, aya 32

43:32

أَهُمۡ يَقۡسِمُونَ رَحۡمَتَ رَبِّكَۚ نَحۡنُ قَسَمۡنَا بَيۡنَهُم مَّعِيشَتَهُمۡ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَاۚ وَرَفَعۡنَا بَعۡضَهُمۡ فَوۡقَ بَعۡضٖ دَرَجَٰتٖ لِّيَتَّخِذَ بَعۡضُهُم بَعۡضٗا سُخۡرِيّٗاۗ وَرَحۡمَتُ رَبِّكَ خَيۡرٞ مِّمَّا يَجۡمَعُونَ ٣٢

Ahum yaqsimūna rahmata rabbika nahnu qasamnā baynahum ma'īshatahum fil-hayawātid-dunyā warafa'nā ba'dahum fawqa ba'din darajātil liyattakhidha ba'duhum ba'dan sukhriyyan warahmatu rabbika khayrum mimmā yajma'ūn

Kwani wao ndio wanao gawa rehema za Mola wako Mlezi? Sisi tumewagawanyia baina yao maisha yao katika uhai wa duniani, na tukawanyanyua baadhi yao juu ya wengine kwa daraja nyingi; kwa hivyo baadhi yao wanawafanya wenginewe wawatumikie. Na rehema za Mwenyezi Mungu ni bora kuliko hayo wanayo yakusanya. 32

Maelezo ya chini

32 Funguo za Utume hazimo katika mikono ya washirikina, hata wao wawakabidhi watu wenye vyeo. Sisi tumewapangia maisha yao kwa kuwa wao wenyewe hawajiwezi. Na tumewafadhilisha baadhi juu ya wengine katika riziki na vyeo, na kwa hivyo baadhi yao huwafanya wengineo wawasaidie na wawatumikie katika kutimiza haja zao, ili wategemeane katika kutafuta maisha na kupanga uhai. Na Unabii na yaliyo khusiana nayo katika neema za Akhera na dunia, ni bora kuliko vyeo vyote vya duniani.