أَمِ ٱتَّخَذَ مِمَّا يَخۡلُقُ بَنَاتٖ وَأَصۡفَىٰكُم بِٱلۡبَنِينَ ١٦
Amit-takhadha mimmā yakhluqu banātin wa asfākum bil-banīn
Au amejichukulia watoto wanawake katika vile alivyo viumba, na akakuteulieni nyinyi watoto wanaume? 16
Maelezo ya chini
16 Ati mnadai kwamba Yeye amejitwalia katika viumbe vyake watoto wa kike, na nyinyi akakukhiarieni watoto wanaume? Ama hakika haya ni mambo ya ajabu kweli!