عَفَا ٱللَّهُ عَنكَ لِمَ أَذِنتَ لَهُمۡ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكَ ٱلَّذِينَ صَدَقُواْ وَتَعۡلَمَ ٱلۡكَٰذِبِينَ ٤٣
'Afallāhu 'anka lima adhinta lahum hattā yatabayyana lakal-ladhīna sadaqū wata'lamal-kādhibīn
Mwenyezi Mungu amekusamehe! Kwa nini ukawapa ruhusa kabla ya kubainikia kwako wanao sema kweli, na ukawajua waongo? 43
Maelezo ya chini
43 Mwenyezi Mungu amekusamehe, ewe Mtume, kwa kuwaruhusu hawa wanaafiki wabaki nyuma wasende kwenye Jihadi kabla ya kuwa haijabainika kwako ukajua kwamba udhuru wao ni wa kweli, na kuwajua walio waongo kati yao katika madai yao kuwa wanaamini, na kuwa ati wana udhuru za kweli..