يُرِيدُونَ أَن يُطۡفِـُٔواْ نُورَ ٱللَّهِ بِأَفۡوَٰهِهِمۡ وَيَأۡبَى ٱللَّهُ إِلَّآ أَن يُتِمَّ نُورَهُۥ وَلَوۡ كَرِهَ ٱلۡكَٰفِرُونَ ٣٢
Yurīdūna an yutfi'ū nūrallāhi bi afwāhihim waya'ballāhu illā an yutimma nūrahū walaw karihal-kāfirūn
Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, na Mwenyezi Mungu anakataa ila aitimize Nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia. 32
Maelezo ya chini
32 Makafiri wanataka kwa madai yao ya upotovu waizime Nuru ya Mwenyezi Mungu, nayo ni Uislamu. Na Mwenyezi Mungu hataki ila aitimize Nuru yake, kwa kuidhihirisha Dini yake na ashinde Mtume wake, ijapo kuwa wao watachukia.