وَأَذَٰنٞ مِّنَ ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦٓ إِلَى ٱلنَّاسِ يَوۡمَ ٱلۡحَجِّ ٱلۡأَكۡبَرِ أَنَّ ٱللَّهَ بَرِيٓءٞ مِّنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ وَرَسُولُهُۥۚ فَإِن تُبۡتُمۡ فَهُوَ خَيۡرٞ لَّكُمۡۖ وَإِن تَوَلَّيۡتُمۡ فَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّكُمۡ غَيۡرُ مُعۡجِزِي ٱللَّهِۗ وَبَشِّرِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ ٣
Wa adhānum minallāhi warasūlihī ilan-nāsi yawmal-hajjil-akbari annallāha barī'um minal-mushrikīna warasūluhū fa in tubtum fahuwa khayrul lakum wa in tawallaytum fa'lamū annakum ghayru mu'jizillāhi wabasshiril-ladhīna kafarū bi'adhābin alīm
Na ni tangazo kutokana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa wote siku ya Hija Kubwa kwamba Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawana jukumu lolote kwa washirikina. Basi mkitubu itakuwa kheri kwenu, na mkigeuka basi jueni kuwa nyinyi hamumshindi Mwenyezi Mungu. Na wabashirie makafiri kuwa watapata adhabu chungu. 3
Maelezo ya chini
3 Na hili ni Tangazo linalo toka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake kuwatangazia watu wote wanapo jumuika siku ya Hija Kubwa ya kwamba:- Hakika Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanajitoa katika dhima, au jukumu, yoyote katika mapatano na washirikina walio fanya khiana. Basi enyi washirikina, mlio vunja ahadi! Mkirudi mkaacha kumshirikisha Mwenyezi Mungu, itakuwa kheri kwenu hapa duniani na kesho Akhera. Lakini mkipuuza na mkabakia hivyo hivyo mlivyo, basi jueni kuwa nyinyi mngali chini ya utawala wa Mwenyezi Mungu. Ewe Mtume! Waonye makafiri wote kuwa ipo adhabu kali yenye uchungu.