Surat At-Tawbah, aya 24

9:24

قُلۡ إِن كَانَ ءَابَآؤُكُمۡ وَأَبۡنَآؤُكُمۡ وَإِخۡوَٰنُكُمۡ وَأَزۡوَٰجُكُمۡ وَعَشِيرَتُكُمۡ وَأَمۡوَٰلٌ ٱقۡتَرَفۡتُمُوهَا وَتِجَٰرَةٞ تَخۡشَوۡنَ كَسَادَهَا وَمَسَٰكِنُ تَرۡضَوۡنَهَآ أَحَبَّ إِلَيۡكُم مِّنَ ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَجِهَادٖ فِي سَبِيلِهِۦ فَتَرَبَّصُواْ حَتَّىٰ يَأۡتِيَ ٱللَّهُ بِأَمۡرِهِۦۗ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡفَٰسِقِينَ ٢٤

Qul in kāna ābā'ukum wa abnā'ukum wa ikhwānukum wa azwājukum wa'ashīratukum wa amwāluniqtaraftumūhā watijāratun takhshawna kasādahā wamasākinu tardawnahā ahabba ilaykum minallāhi warasūlihī wajihādin fī sabīlihī fatarabbasū hattā ya'tiyallāhu bi amrihī wallāhu lā yahdil-qawmal-fāsiqīn

Sema: Ikiwa baba zenu, na wenenu, na ndugu zenu, na wake zenu, na jamaa zenu, na mali mliyo yachuma, na biashara mnazo ogopa kuharibika, na majumba mnayo yapenda, ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Jihadi katika Njia yake, basi ngojeni mpaka Mwenyezi Mungu alete amri yake. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wapotovu. 24

Maelezo ya chini

24 Ewe Mtume! Waambie Waumini: Ikiwa baba zenu, na ndugu zenu, na wake zenu, na jamaa zenu, na mali mliyo yachuma, na biashara mnazo khofu zisibwage, na majumba mnayo starehea kuyakaa, mnayapenda zaidi kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume na Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, hata mkaacha kumuunga mkono Mtume, basi ngojeni mpaka Mwenyezi Mungu akuleteeni hukumu yake na adhabu yake. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi wenye kutoka kwenye mipaka ya Dini yake.