Surat At-Tawbah, aya 13

9:13

أَلَا تُقَٰتِلُونَ قَوۡمٗا نَّكَثُوٓاْ أَيۡمَٰنَهُمۡ وَهَمُّواْ بِإِخۡرَاجِ ٱلرَّسُولِ وَهُم بَدَءُوكُمۡ أَوَّلَ مَرَّةٍۚ أَتَخۡشَوۡنَهُمۡۚ فَٱللَّهُ أَحَقُّ أَن تَخۡشَوۡهُ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ ١٣

Alā tuqātilūna qawman nakathū aymānahum wahammū bi ikhrājir-rasūli wahum bada'ūkum awwala marratin atakhshawnahum fallāhu ahaqqu an takhshawhu in kuntum mu'minīn

Je, hamtapigana na watu walio vunja viapo vyao na wakawa na hamu ya kumfukuza Mtume, nao ndio walio kuanzeni mara ya kwanza? Je, mnawaogopa? Basi Mwenyezi Mungu anastahiki zaidi mumwogope, ikiwa nyinyi ni Waumini. 13

Maelezo ya chini

13 Enyi Waumini! Kwa nini msikimbilie kwenda vitani kuwapiga vita washirikina walio vunja mapatano yenu mara kwa mara, na wao walikuwa wakijihimu kumfukuza Mtume Makka na kumuuwa, na wao tena ndio walio kuanzeni kukuteseni na kukufanyieni uadui tangu mwanzo? Je, mnawaogopa? Msiwaogope! Mwenyezi Mungu tu peke yake ndiye anaye stahiki nyinyi mumwogope, kama nyinyi ni wakweli katika Imani yenu.