Surat At-Tawbah, aya 129

9:129

فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَقُلۡ حَسۡبِيَ ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۖ عَلَيۡهِ تَوَكَّلۡتُۖ وَهُوَ رَبُّ ٱلۡعَرۡشِ ٱلۡعَظِيمِ ١٢٩

Fa in tawallaw faqul hasbiyallāhu lā ilāha illā huwa 'alayhi tawakkaltu wahuwa rabbul-'arshil-'azīm

Basi wakigeuka, wewe sema: Mwenyezi Mungu ananitosheleza. Hapana mungu isipokuwa Yeye tu. Mimi namtegemea Yeye, na Yeye ndiye Mola Mlezi wa Kiti Kikuu cha Enzi. 129

Maelezo ya chini

129 Basi, ewe Mtume! Wakiipuuza Imani, wakaikataa, wewe usihuzunike kwa mapuuza yao. Wewe tafakhari na utukufu wa Mola wako Mlezi, na useme: Ananitosheleza Mwenyezi Mungu, ambaye hapana mungu asiye kuwa Yeye. Juu yake Yeye tu peke yake mimi nategemea. Na Yeye ndiye Mmiliki wa ufalme wote, Mola Mlezi wa viumbe vyote, na ndiye Mwenye utawala mkuu.