Surat At-Tahrim, aya 10

66:10

ضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلٗا لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ ٱمۡرَأَتَ نُوحٖ وَٱمۡرَأَتَ لُوطٖۖ كَانَتَا تَحۡتَ عَبۡدَيۡنِ مِنۡ عِبَادِنَا صَٰلِحَيۡنِ فَخَانَتَاهُمَا فَلَمۡ يُغۡنِيَا عَنۡهُمَا مِنَ ٱللَّهِ شَيۡـٔٗا وَقِيلَ ٱدۡخُلَا ٱلنَّارَ مَعَ ٱلدَّٰخِلِينَ ١٠

Daraballāhu mathalal lilladhīna kafarumra'ata nūhin wamra'ata lūtin kānatā tahta 'abdayni min 'ibādinā sālihayni fakhānatāhumā falam yughniyā 'anhumā minallāhi shay'an waqīladkhulan-nāra ma'ad-dākhilīn

Mwenyezi Mungu amewapigia mfano walio kufuru: mke wa Nuhu na mke wa Lut'i. Walikuwa chini ya waja wetu wema wawili miongoni mwa waja wetu. Lakini wakawakhuni waume zao, nao wasiwafae kitu. Na ikasemwa: Ingieni Motoni pamoja na wanao ingia! 10

Maelezo ya chini

10 Mwenyezi Mungu ametaja hali ya ajabu inayo juulikana kuwa ni hali zinazo fanana kwa wanao kufuru. Nayo ni hali ya mke wa Nuhu na mke wa Lut'i. Hao walikuwa chini ya ulinzi wa waja wawili katika waja wema. Nao wakawakhuni kwa kupanga njama dhidi yao, na kufichua siri zao kwenda wambia kaumu zao. Na waja wema wawili hawakuweza kuwakinga wake zao kwa lolote katika adhabu ya Mwenyezi Mungu. Na wakaambiwa hao wake wawili walipo angamizwa: Ingieni Motoni pamoja na wanao ingia!