فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ مَا ٱسۡتَطَعۡتُمۡ وَٱسۡمَعُواْ وَأَطِيعُواْ وَأَنفِقُواْ خَيۡرٗا لِّأَنفُسِكُمۡۗ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفۡسِهِۦ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ ١٦
Fattaqullāha mastata'tum wasma'ū wa atī'ū wa anfiqū khayral li anfusikum waman yūqa shuhha nafsihī fa ulā'ika humul-muflihūn
Basi mcheni Mwenyezi Mungu kama mwezavyo, na sikieni, na t'iini, na toeni, itakuwa kheri kwa nafsi zenu. Na mwenye kuepushwa na uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio walio fanikiwa. 16
Maelezo ya chini
16 Basi tumieni juhudi zenu na nguvu zenu katika kumcha Mwenyezi Mungu. Na sikieni mawaidha yake, na t'iini amri zake, na toeni katika alicho kuruzukuni kwa ajili ya hicho alicho amrisha kitolewe kwa ajili yake. Na tendeni kheri kwa sababu ya nafsi zenu. Na mwenye kuzuiliwa na Mwenyezi Mungu ubakhili na uchoyo wa roho yake, basi watu kama hao ndio walio jaaliwa kupata kila kheri.