ٱللَّهُ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَمَا بَيۡنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٖ ثُمَّ ٱسۡتَوَىٰ عَلَى ٱلۡعَرۡشِۖ مَا لَكُم مِّن دُونِهِۦ مِن وَلِيّٖ وَلَا شَفِيعٍۚ أَفَلَا تَتَذَكَّرُونَ ٤
Allāhul-ladhī khalaqas-samāwāti wal-arda wamā baynahumā fī sittati ayyāmin thummastawā 'alal-'arshi mā lakum min dūnihī min waliyyin walā shafī'in afalā tatadhakkarūn
Mwenyezi Mungu ndiye aliye umba mbingu na ardhi na viliomo baina yao kwa siku sita, na akatawala kwenye Kiti cha Enzi. Nyinyi hamna mlinzi wala mwombezi isipo kuwa Yeye tu. Basi, je, hamkumbuki? 4
Maelezo ya chini
4 Mwenyezi Mungu aliye umba mbingu na ardhi na vilio baina yao kwa siku sita, kisha akatawala juu ya Kiti cha Enzi, A'rshi, kwa utawala ulio laiki naye. Nyinyi hamna badala yake Yeye yeyote msaidizi wa kukunusuruni, wala mwombezi wa kukuombeeni. Basi je, mtaendelea kushikilia kuwa katika ukafiri na inda, wala msiwaidhike kwa mawaidha ya Mwenyezi Mungu?