Surat Ar-Ra'd, aya 7

13:7

وَيَقُولُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَوۡلَآ أُنزِلَ عَلَيۡهِ ءَايَةٞ مِّن رَّبِّهِۦٓۗ إِنَّمَآ أَنتَ مُنذِرٞۖ وَلِكُلِّ قَوۡمٍ هَادٍ ٧

Wayaqūlul-ladhīna kafarū lawlā unzila 'alayhi āyatum mir rabbihī innamā anta mundhirun walikulli qawmin hād

Na wale walio kufuru husema: Mbona hakuteremshiwa muujiza kutoka kwa Mola wake Mlezi? Hakika wewe ni Mwonyaji, na kila kaumu ina wa kuwaongoa. 7

Maelezo ya chini

7 Na husema hao makafiri wasio amini muujiza mkubwa, yaani Qur'ani: Hebu na amteremshie Mola wake Mlezi alama ya unabii wake wa kuonekana kama kuiendesha milima akawa Mwenyezi Mungu anaonyesha wazi uhakika wa Nabii wake katika jambo hili! Na Yeye Subhanahu anamwambia: Hakika wewe ni Nabii wa kuwaonya kwamba kuna adhabu mbaya wakiendelea na upotovu wao. Na kila kaumu wanaye Mtume wa kuwaongoza kwenye Haki, na muujiza wa kubainisha ujumbe wake. Si wao wa kuchagua. Lao ni kujibu upinzani na kuleta mfano wake!