Surat Ar-Ra'd, aya 11

13:11

لَهُۥ مُعَقِّبَٰتٞ مِّنۢ بَيۡنِ يَدَيۡهِ وَمِنۡ خَلۡفِهِۦ يَحۡفَظُونَهُۥ مِنۡ أَمۡرِ ٱللَّهِۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوۡمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُواْ مَا بِأَنفُسِهِمۡۗ وَإِذَآ أَرَادَ ٱللَّهُ بِقَوۡمٖ سُوٓءٗا فَلَا مَرَدَّ لَهُۥۚ وَمَا لَهُم مِّن دُونِهِۦ مِن وَالٍ ١١

Lahū mu'aqqibātum mim bayni yadayhi wamin khalfihī yahfazūnahū min amrillāhi innallāha lā yughayyiru mā biqawmin hattā yughayyirū mā bi anfusihim wa idhā arādallāhu biqawmin sū'an falā maradda lahū wamā lahum min dūnihī min wāl

Kila mtu analo kundi la malaika mbele yake na nyuma yake linamlinda kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo naf- sini mwao. Na Mwenyezi Mungu anapo watakia watu adhabu hakuna cha kuzuia wala hawana mlinzi yeyote badala yake. 11

Maelezo ya chini

11 Na Mwenyezi Mungu Aliye takasika ndiye anaye kuhifadhini. Kila mtu anao Malaika wanao mlinda kwa amri ya Mwenyezi Mungu, na wanapeana zamu kumlinda mbele na nyuma yake. Na hakika Mwenyezi Mungu Subhanahu habadilishi hali ya watu kutoka shida kwendea neema, na kutoka nguvu wakawa dhaifu, mpaka wao wenyewe wageuze waliyo nayo kufuatana na hali wanayo iendea. Na Mwenyezi Mungu akitaka kuwateremshia watu maovu basi hawana wa kuwanusuru ataye walinda na amri yake, wala wa kuwatazamia mambo yao kuwakinga na yatayo wateremkia.