Surat An-Nur, aya 54

24:54

قُلۡ أَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُواْ ٱلرَّسُولَۖ فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَإِنَّمَا عَلَيۡهِ مَا حُمِّلَ وَعَلَيۡكُم مَّا حُمِّلۡتُمۡۖ وَإِن تُطِيعُوهُ تَهۡتَدُواْۚ وَمَا عَلَى ٱلرَّسُولِ إِلَّا ٱلۡبَلَٰغُ ٱلۡمُبِينُ ٥٤

Qul atī'ullāha wa atī'ur-rasūla fa in tawallaw fa innamā 'alayhi mā hummila wa'alaykum mā hummiltum wa in tutī'ūhu tahtadū wamā 'alar-rasūli illal-balāghul-mubīn

Sema: Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume. Na mkigeuka, basi yaliyo juu yake ni aliyo bebeshwa, na yaliyo juu yenu ni mliyo bebshwa nyinyi. Na mkimt'ii yeye mtaongoka. Na hapana juu ya Mtume ila kufikisha Ujumbe wazi wazi. 54

Maelezo ya chini

54 Waambie: Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume kwa ut'iifu wa kweli wenye kuonyesha vitendo vyenu. Wanaafiki wakipuuza wasifuate, basi juu ya Muhammad ni waajibu wa aliyo twishwa tu na Mwenyezi Mungu, nayo ni amri ya kufikilisha Ujumbe, wala hakukalifishwa uwongofu wao. Na nyinyi juu yenu ni hayo aliyo kutwikeni Mwenyezi Mungu nayo ni kufuata na kut'ii. Na mtapata adhabu ikiwa mtaendelea na uasi. Na mkimt'ii Mtume mtaongoka kwenye kheri. Na yeye haimpasi ila kufikisha kwa uwazi mukimti au mukiamsi na yeye akaisha fikisha