Surat An-Nur, aya 53

24:53

۞ وَأَقۡسَمُواْ بِٱللَّهِ جَهۡدَ أَيۡمَٰنِهِمۡ لَئِنۡ أَمَرۡتَهُمۡ لَيَخۡرُجُنَّۖ قُل لَّا تُقۡسِمُواْۖ طَاعَةٞ مَّعۡرُوفَةٌۚ إِنَّ ٱللَّهَ خَبِيرُۢ بِمَا تَعۡمَلُونَ ٥٣

Wa aqsamū billāhi jahda aymānihim la in amartahum layakhrujunna qul lā tuqsimū tā'atum ma'rūfatun innallāha khabīru bimā ta'malūn

Na wanaapa kwa Mwenyezi Mungu ukomo wa kiapo chao ya kwamba ukiwaamrisha kwa yakini watatoka. Sema: Msiape! Ut'iifu unajuulikana. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda. 53

Maelezo ya chini

53 Na wanaafiki wanaapa kwa ukomo wa nguvu za viapo vyao, kwamba wewe, Muhammad, ukiwaamrisha watoke nawe kwenda vitani watakut'ii. Waambie: Msiape! Kwani mambo yatakikanayo kwenu mnayajua, hapana hata mmoja wenu asiye yajua. Wala yamini zenu za uwongo haziondoi ujuzi huo. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua baraabara kila linalo tokana nanyi, na Yeye atakulipeni kwayo.