Surat An-Nur, aya 42

24:42

وَلِلَّهِ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ وَإِلَى ٱللَّهِ ٱلۡمَصِيرُ ٤٢

Walillāhi mulkus-samāwāti wal-ardi wa ilallāhil-masīr

Na ni wa Mwenyezi Mungu ufalme wa mbingu na ardhi, na kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo ya wote. 42

Maelezo ya chini

42 Na Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Mwenye kumiliki mbingu na ardhi na viliomo ndani yao, na ndiye Mwenye madaraka juu yao, na wote watarejea kwake Siku ya Kiyama kwa ajili ya hisabu na malipo.