وَأَنكِحُواْ ٱلۡأَيَٰمَىٰ مِنكُمۡ وَٱلصَّٰلِحِينَ مِنۡ عِبَادِكُمۡ وَإِمَآئِكُمۡۚ إِن يَكُونُواْ فُقَرَآءَ يُغۡنِهِمُ ٱللَّهُ مِن فَضۡلِهِۦۗ وَٱللَّهُ وَٰسِعٌ عَلِيمٞ ٣٢
Wa ankihul-ayāmā minkum was-sālihīna min 'ibādikum wa imā'ikum in yakūnū fuqarā'a yughnihimullāhu min fadlihī wallāhu wāsi'un 'alīm
Na waozeni wajane miongoni mwenu na wema katika watumwa wenu na wajakazi wenu. Wakiwa mafakiri Mwenyezi Mungu atawatajirisha kwa fadhila yake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa Mwenye kujua. 32
Maelezo ya chini
32 Na saidieni katika kujitenga na zina na yanayo pelekea zina, kwa kuwaoza ambao bado hawajaoana miongoni mwa wanaume wenu na wanawake wenu, na walio kuwa wanafaa kwa hayo katika watumwa wenu. Na wala umasikini usiwe sababu ya kuzuilia kuoa. Kwani Mwenyezi Mungu atasahilisha njia za maisha mazuri kwa mwenye kutaka kuishi maisha safi. Na fadhila za Mwenyezi Mungu ni kunjufu, na Yeye anajua kabisa niya za watu, na kila lipitalo katika ulimwengu.