Surat An-Nur, aya 30

24:30

قُل لِّلۡمُؤۡمِنِينَ يَغُضُّواْ مِنۡ أَبۡصَٰرِهِمۡ وَيَحۡفَظُواْ فُرُوجَهُمۡۚ ذَٰلِكَ أَزۡكَىٰ لَهُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ خَبِيرُۢ بِمَا يَصۡنَعُونَ ٣٠

Qul lil-mu'minīna yaghuddū min absārihim wayahfazū furūjahum dhālika azkā lahum innallāha khabīru bimā yasna'ūn

Waambie Waumini wanaume wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao. Hili ni takaso bora kwao. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za wanayo yafanya. 30

Maelezo ya chini

30 Ewe Nabii! Waambie Waumini katika yanayo pelekea zina na kutilisha shaka, wasitazame yanayo harimishwa kutazama, nayo ni tupu za wanawake na sehemu za uzuri wao, na wanaume wahifadhi tupu zao kwa kuzisitiri na kuto zitumilia kwa njia isiyo ruhusiwa na Sharia. Adabu hiyo ndio ina hishima zaidi na safi zaidi kwao wasiingie katika maasi na tuhuma. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua baraabara yote wayatendayo, na atakuja walipa kwayo.