Surat An-Nur, aya 15

24:15

إِذۡ تَلَقَّوۡنَهُۥ بِأَلۡسِنَتِكُمۡ وَتَقُولُونَ بِأَفۡوَاهِكُم مَّا لَيۡسَ لَكُم بِهِۦ عِلۡمٞ وَتَحۡسَبُونَهُۥ هَيِّنٗا وَهُوَ عِندَ ٱللَّهِ عَظِيمٞ ١٥

Idh talaqqawnahū bi alsinatikum wataqūlūna bi afwāhikum mā laysa lakum bihī 'ilmun watahsabūnahū hayyinan wahuwa 'indallāhi 'azīm

Mlipo yapokea kwa ndimi zenu na mkasema kwa vinywa vyenu msiyo yajua, na mlifikiri ni jambo dogo, kumbe mbele ya Mwenyezi Mungu ni kubwa. 15

Maelezo ya chini

15 Mmezichukua khabari hizo kwa ndimi zenu na mkazieneza kati yenu. Wala nyinyi hamkujua kuwa hizo ni khabari za kweli, na mkaona jambo hili ni dogo si la kuadhibiwa na Mwenyezi Mungu, au sana adhabu yake ni ndogo; na ilhali ni jambo kubwa kweli la kuadhibiwa adhabu kali na Mwenyezi Mungu.