إِنَّ ٱلَّذِينَ جَآءُو بِٱلۡإِفۡكِ عُصۡبَةٞ مِّنكُمۡۚ لَا تَحۡسَبُوهُ شَرّٗا لَّكُمۖ بَلۡ هُوَ خَيۡرٞ لَّكُمۡۚ لِكُلِّ ٱمۡرِيٕٖ مِّنۡهُم مَّا ٱكۡتَسَبَ مِنَ ٱلۡإِثۡمِۚ وَٱلَّذِي تَوَلَّىٰ كِبۡرَهُۥ مِنۡهُمۡ لَهُۥ عَذَابٌ عَظِيمٞ ١١
Innal-ladhīna jā'ū bil-ifki 'usbatum minkum lā tahsabūhu sharral lakum bal huwa khayrul lakum likullimriy'im minhum maktasaba minal-ithmi walladhī tawallā kibrahū minhum lahū 'adhābun 'azīm
Hakika wale walio leta uwongo ni kundi miongoni mwenu. Msifikiri ni shari kwenu, bali hiyo ni kheri kwenu. Kila mtu katika wao atapata aliyo yachuma katika madhambi. Na yule aliyejitwika sehemu yake kubwa miongoni mwao, atapata adhabu kubwa. 11
Maelezo ya chini
11 Hakika hao walio zua uwongo ulio potoka na kila uwongofu kumzulia Aisha, mke wa Nabii s.a.w. walipo mtangazia uzushi, ni kikundi wanao ishi pamoja nanyi. Msidhani kituko hichi ni shari kwenu, bali ndiyo kheri yenu; kwa sababu kimewapambanua baina ya wanaafiki na Waumini wa kweli. Na ukadhihiri ukarimu wa walio wema na wenye kuingiwa na uchungu. Na kila mtu katika hawa walio tuhumu watapata malipo yao kwa mujibu wa kadri alivyo shiriki katika uzushi huu. Na mkuu wa kikundi hichi ndiye ataye pata adhabu kubwa kwa ukubwa wa makosa yake.