وَإِذَا حُيِّيتُم بِتَحِيَّةٖ فَحَيُّواْ بِأَحۡسَنَ مِنۡهَآ أَوۡ رُدُّوهَآۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٍ حَسِيبًا ٨٦
Wa idhā huyyītum bitahiyyatin fahayyū bi ahsana minhā aw ruddūhā innallāha kāna 'alā kulli shay'in hasībā
Na mnapo amkiwa kwa maamkio yoyote, basi nanyi itikieni kwa yaliyo bora kuliko hayo, au rejesheni hayo hayo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuhisabu kila kitu. 86
Maelezo ya chini
86 Akikuamkieni mtu yeyote kwa maamkio ya salamu, au dua, au ya namna yoyote ya hishima, au namna nyengine yoyote ile, basi mjibuni kwa maamkio yaliyo mazuri zaidi, au kwa uchache mjibuni kama alivyo kuamkieni yeye. Kwani hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kutia hisabuni kila kitu, kikubwa na kidogo.