وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ سَنُدۡخِلُهُمۡ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدٗاۖ لَّهُمۡ فِيهَآ أَزۡوَٰجٞ مُّطَهَّرَةٞۖ وَنُدۡخِلُهُمۡ ظِلّٗا ظَلِيلًا ٥٧
Walladhīna āmanū wa'amilus-sālihāti sanudkhiluhum jannātin tajrī min tahtihal-anhāru khālidīna fīhā abadal lahum fīhā azwājum mutahharatun wanudkhiluhum zillan zalīlā
Na wale walio amini na wakatenda mema tutawaingiza katika Pepo zipitazo mito kati yake kwa kudumu humo milele. Huko watakuwa na wake walio takasika, na tutawaingiza katika vivuli vizuri kweli. 57
Maelezo ya chini
57 Na ambao walio yasadiki yaliyo wajia kutoka kwa Mola wao Mlezi, na wakatenda vitendo vyema, tutawalipa kwa Imani yao na vitendo vyao na tutawaingiza katika Mabustani ya Peponi yapitayo mito chini ya miti yake. Uhai wao hauna kikomo kabisa. Nao humo watakuwa na wake walio t'ahirika na kila la aibu na uchafu. Tutawapa uhai wa starehe chini ya vivuli vizuri vya kudumu, waishi maisha mema yenye neema isiyo kwisha.