فَمِنۡهُم مَّنۡ ءَامَنَ بِهِۦ وَمِنۡهُم مَّن صَدَّ عَنۡهُۚ وَكَفَىٰ بِجَهَنَّمَ سَعِيرًا ٥٥
Faminhum man āmana bihī waminhum man sadda 'anhu wakafā bijahannama sa'īrā
Basi wapo miongoni mwao waliyo yaamini, na wapo walio yakataa. Na Jahannamu yatosha kuwa ni moto wa kuwateketeza. 55
Maelezo ya chini
55 Miongoni mwa walio pelekewa Nabii Ibrahim na ukoo wake wapo wenye kukiamini Kitabu kilicho teremshiwa kwao, na wapo walio kipa nyongo wakajitenga nacho. Na jaza ya hawa wenye kujitenga na wito wa Haki ni Jahannamu yenye moto wa kuteketeza.