Surat An-Nisa, aya 4

4:4

وَءَاتُواْ ٱلنِّسَآءَ صَدُقَٰتِهِنَّ نِحۡلَةٗۚ فَإِن طِبۡنَ لَكُمۡ عَن شَيۡءٖ مِّنۡهُ نَفۡسٗا فَكُلُوهُ هَنِيٓـٔٗا مَّرِيٓـٔٗا ٤

Wa ātun-nisā'a saduqātihinna nihlatan fa in tibna lakum 'an shay'im minhu nafsan fakulūhu hanī'an mmarī'ā

Na wapeni wanawake mahari yao hali ya kuwa ni kipawa. Lakini wakikutunukieni kitu katika mahari, kwa radhi yao, basi kileni kiwashuke kwa raha. 4

Maelezo ya chini

4 Wapeni wanawake mahari yao kuwa ni kipawa, tunza iliyo safi. Na nyinyi hamna haki yoyote katika hayo mahari. Ikiwa hao wanawake kwa radhi ya nafsi zao wenyewe wakakubali kusamehe sehemu yoyote ya mahari mliyo kwisha ahadiana, basi hapo mnayo ruhusa kuchukua na mkatumia kwa kheri na salama.