فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ بِٱللَّهِ وَٱعۡتَصَمُواْ بِهِۦ فَسَيُدۡخِلُهُمۡ فِي رَحۡمَةٖ مِّنۡهُ وَفَضۡلٖ وَيَهۡدِيهِمۡ إِلَيۡهِ صِرَٰطٗا مُّسۡتَقِيمٗا ١٧٥
Fa ammal-ladhīna āmanū billāhi wa'tasamū bihī fasayudkhiluhum fī rahmatim minhu wafadlin wayahdīhim ilayhi sirātam mustaqīmā
Ama wale walio muamini Mwenyezi Mungu, na wakashikamana naye, basi atawatia katika rehema yake na fadhila, na atawaongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka. 175
Maelezo ya chini
175 Ama walio msadiki Mwenyezi Mungu na ujumbe wake alio leta, na wakaifuata Dini yake, atawatia katika Bustani zake Akhera, na atawamiminia rehema yake, na atawakusanya katika ukunjufu wa fadhila yake, na atawawezesha hapa duniani kuthibiti katika Njia yake Iliyo Nyooka.