إِن يَشَأۡ يُذۡهِبۡكُمۡ أَيُّهَا ٱلنَّاسُ وَيَأۡتِ بِـَٔاخَرِينَۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلَىٰ ذَٰلِكَ قَدِيرٗا ١٣٣
In yasha' yudhhibkum ayyuhan-nāsu waya'ti bi'ākharīna wakānallāhu 'alā dhālika qadīrā
Akitaka atakuondoeni, enyi watu! Na awalete wengineo. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa hayo. 133
Maelezo ya chini
133 Hakika nyinyi enyi waja wa Mwenyezi Mungu! Mko chini ya ufalme wa Mwenyezi Mungu Mwenye uweza na Mwenye nguvu. Akipenda atakufisheni na alete wengine kabisa. Na Yeye Mwingi wa Utukufu ni Muweza wa hayo, na Muweza wa kila kitu.