وَمَن يَعۡمَلۡ مِنَ ٱلصَّٰلِحَٰتِ مِن ذَكَرٍ أَوۡ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤۡمِنٞ فَأُوْلَٰٓئِكَ يَدۡخُلُونَ ٱلۡجَنَّةَ وَلَا يُظۡلَمُونَ نَقِيرٗا ١٢٤
Waman ya'mal minas-sālihāti min dhakarin aw unthā wahuwa mu'minun fa ulā'ika yadkhulūnal-jannata walā yuzlamūna naqīrā
Na anaye fanya mema, akiwa mwanamume au mwanamke, naye ni Muumini - basi hao wataingia Peponi wala hawatadhulumiwa hata kadiri ya tundu ya kokwa ya tende. 124
Maelezo ya chini
124 Watendao mema, kwa kadiri ya uwezo wao nao wanamuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wataingia kwenye Pepo ya neema, wala hawatapunguziwa hata chembe. Na hapana khitilafu baina ya malipo ya mwanamume na ya mwanamke, kwani mwanamke naye ana waajibu wake, malipo ya vitendo vyema, na adhabu kwa vitendo vibaya.