Surat An-Naml, aya 86

27:86

أَلَمۡ يَرَوۡاْ أَنَّا جَعَلۡنَا ٱلَّيۡلَ لِيَسۡكُنُواْ فِيهِ وَٱلنَّهَارَ مُبۡصِرًاۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ ٨٦

Alam yaraw annā ja'alnal-layla liyaskunū fīhi wan-nahāra mubsiran inna fī dhālika la'āyātil liqawmin yu'minūn

Je! Hawaoni kwamba sisi tumeufanya usiku ili watulie, na mchana wa kuangaza. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa watu wanao amini. 86

Maelezo ya chini

86 Bila ya shaka wameshuhudia kuwa Mwenyezi Mungu ameufanya usiku ili wapate kupumzika, na akaufanya mchana una mwangaza, wapate kushughulikia kutafuta maisha yao. Hakika katika hayo zipo dalili wazi za Ungu wa Mwenyezi Mungu, na Upweke wake, kwa watu wanao zingatia wakaamini.