Surat An-Naml, aya 84

27:84

حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءُو قَالَ أَكَذَّبۡتُم بِـَٔايَٰتِي وَلَمۡ تُحِيطُواْ بِهَا عِلۡمًا أَمَّاذَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ ٨٤

Hattā idhā jā'ū qāla akaddhabtum bi'āyātī walam tuhītū bihā 'ilman ammādhā kuntum ta'malūn

Hata watakapo fika, atasema (Mwenyezi Mungu): Je! Nyinyi si mlizikanusha Ishara zangu pasipo kuzijua vyema? Au mlikuwa mkifanya nini? 84

Maelezo ya chini

84 Na pale watakapo simama mbele ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya hisabu, atasema Subhanahu kuwaambia kwa kuwadhili na kuwabinya: Nyinyi mlizikadhibisha Ishara zangu zote, na mkazikataa bila ya kuzingatia wala kufahamu. Na khasa mlikuwa mkitenda nini nanyi hamkuumbwa kwa upuuzi?