تَٱللَّهِ لَقَدۡ أَرۡسَلۡنَآ إِلَىٰٓ أُمَمٖ مِّن قَبۡلِكَ فَزَيَّنَ لَهُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ أَعۡمَٰلَهُمۡ فَهُوَ وَلِيُّهُمُ ٱلۡيَوۡمَ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ ٦٣
Tallāhi laqad arsalnā ilā umamim min qablika fazayyana lahumush-shaytānu a'mālahum fahuwa waliyyuhumul-yawma walahum 'adhābun alīm
Wallahi! Sisi tulituma Mitume kwa umati zilizo kuwa kabla yako,lakini Shetani aliwapambia vitendo vyao. Kwa hivyo leo yeye ndiye rafiki yao; nao watapata adhabu chungu. 63
Maelezo ya chini
63 Ewe Nabii! Jua kwa yakini kwamba Sisi tuliwatuma Mitume kabla yako kwa kaumu nyingi kama tulivyo kutuma wewe kwa watu wote. Lakini Shetani aliwapambia ukafiri, na ushirikina, na maasi. Basi wakawakanya Mitume wao, na wakawaasi, na wakamsadiki Shetani na wakamt'ii yeye. Basi yeye amekuwa ndiye mwenye kuyatawala mambo yao katika dunia, akiwapambia mambo ya kuwadhuru. Na Akhera watapata adhabu yenye machungu makali.