Surat An-Nahl, aya 25

16:25

لِيَحۡمِلُوٓاْ أَوۡزَارَهُمۡ كَامِلَةٗ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ وَمِنۡ أَوۡزَارِ ٱلَّذِينَ يُضِلُّونَهُم بِغَيۡرِ عِلۡمٍۗ أَلَا سَآءَ مَا يَزِرُونَ ٢٥

Liyahmilū awzārahum kāmilatan yawmal-qiyāmati wamin awzāril-ladhīna yudillūnahum bighayri 'ilmin alā sā'a mā yazirūn

Ili wabebe mizigo yao kwa ukamilifu Siku ya Kiyama, na sehemu ya mizigo ya wale wanao wapoteza bila ya kujua. Angalia, ni maovu mno hayo wanayo yabeba! 25

Maelezo ya chini

25 Wanasema hayo ili wawazuie watu wasimfuate Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na mwisho wa kuishia mambo yao ni kuwa wataadhibiwa Siku ya Kiyama kwa adhabu ya upotovu wao kwa ukamilifu, na adhabu ya baadhi ya watu walio kuwa wakiwakhadaa na kuwadanganya mpaka wakapotea bila ya ilimu wala kuchungua! Zingatia, ewe mwenye kusikia, kwa huu uovu wa madhambi wanayo yafanya, vipi ukali wa adhabu watayo pata!