وَعَلَٰمَٰتٖۚ وَبِٱلنَّجۡمِ هُمۡ يَهۡتَدُونَ ١٦
Wa'alāmātin wabin-najmi hum yahtadūn
Na alama nyengine. Na kwa nyota wao wanajiongoza. 16
Maelezo ya chini
16 Na Mwenyezi Mungu ameweka alama za kuwaongoza watu katika safari zao kwenye ardhi, na hivyo wanapata uwongozi katika safari zao kwa nyota ambazo ameziweka mbinguni ziwaongoze wanapo kuwa gizani hawazioni alama za ardhini.