ثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ عَمِلُواْ ٱلسُّوٓءَ بِجَهَٰلَةٖ ثُمَّ تَابُواْ مِنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَ وَأَصۡلَحُوٓاْ إِنَّ رَبَّكَ مِنۢ بَعۡدِهَا لَغَفُورٞ رَّحِيمٌ ١١٩
Thumma inna rabbaka lilladhīna 'amilus-sū'a bijahālatin thumma tābū mim ba'di dhālika wa aslahū inna rabbaka mim ba'dihā laghafūrur rahīm
Kisha hakika Mola wako Mlezi kwa walio tenda uovu kwa ujinga,kisha wakatubia baada ya hayo na wakatenda mema; bila ya shaka Mola wako Mlezi baada ya hayo ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu. 119
Maelezo ya chini
119 Kisha wanao tenda maovu kwa kupitikiwa, au kwa kuacha kuzingatia vilivyo matokeo yatayo tokea, na baadae wakatubia, wakajitengeneza nafsi zao na vitendo vyao, basi hakika Mola wako Mlezi, ewe Nabii, atawasamehe hao madhambi yao. Kwani hakika Yeye Subhanahu baada ya toba hiyo ni Mwingi wa kusamehe madhambi, na ni Mkunjufu wa rehema kwa waja wake.