Surat An-Nahl, aya 111

16:111

۞ يَوۡمَ تَأۡتِي كُلُّ نَفۡسٖ تُجَٰدِلُ عَن نَّفۡسِهَا وَتُوَفَّىٰ كُلُّ نَفۡسٖ مَّا عَمِلَتۡ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ ١١١

Yawma ta'tī kullu nafsin tujādilu 'an nafsihā watuwaffā kullu nafsim mā 'amilat wahum lā yuzlamūn

Siku ambayo kila nafsi itakuja jitetea, na kila nafsi italipwa sawa sawa na a'mali ilizo zifanya, nao hawatadhulumiwa. 111

Maelezo ya chini

111 Ewe Nabii! Watajie watu wako, kwa kuwahadharisha, Siku ambayo kila mtu atakuwa hana linalo mshughulisha ila kujitetea nafsi yake. Hayamshughulishi ya mzazi wala mwana. Siku hiyo ndiyo Siku ya Kiyama! Na Mwenyezi Mungu siku hiyo atailipa kila nafsi malipo ya vitendo iliyo tenda, ikiwa kheri au shari. Na Mola wako Mlezi hamdhulumu hata mtu mmoja.