Surat Al-Qasas, aya 53

28:53

وَإِذَا يُتۡلَىٰ عَلَيۡهِمۡ قَالُوٓاْ ءَامَنَّا بِهِۦٓ إِنَّهُ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّنَآ إِنَّا كُنَّا مِن قَبۡلِهِۦ مُسۡلِمِينَ ٥٣

Wa idhā yutlā 'alayhim qālū āmannā bihī innahul-haqqu mir rabbinā innā kunnā min qablihī muslimīn

Na wanapo somewa wanasema: Tunaiamini. Hakika hii ni Haki inayo toka kwa Mola wetu Mlezi. Hakika sisi kabla yake tulikuwa ni Waislamu, tulio nyenyekea. 53

Maelezo ya chini

53 Na hao wakisomewa Qur'ani hufanya haraka kutangaza Imani yao, na husema: Tumeyaamini hayo, kwani hayo ni Haki inayo toka kwa Mola wetu Mlezi; na sisi tulimjua Muhammad na Kitabu chake hata kabla ya kuteremka kwake, nasi tukanyenyekea kabla ya kusomwa kwake.