Surat Al-Qasas, aya 40

28:40

فَأَخَذۡنَٰهُ وَجُنُودَهُۥ فَنَبَذۡنَٰهُمۡ فِي ٱلۡيَمِّۖ فَٱنظُرۡ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلظَّٰلِمِينَ ٤٠

Fa akhadhnāhu wajunūdahū fanabadhnāhum fil-yammi fanzur kayfa kāna 'āqibatuz-zālimīn

Basi tukamshika yeye na majeshi yake, na tukawatupa baharini. Basi hebu angalia ulikuwaje mwisho wa wenye kudhulumu? 40

Maelezo ya chini

40 Tukamng'oa Firauni kwenye utawala wake, na tukawavutia taratibu yeye na majeshi yake mpaka baharini, na tukawazamisha na huku tunawatupia sababu ya dhulma yao. Basi zingatia, ewe Muhammad, na uwahadharishe watu wako watazame vipi unakuwa mwisho wa wenye kudhulumu katika dunia yao. Na hakika wewe ni mwenye kusaidiwa kupata ushindi juu yao.