وَقَالَ فِرۡعَوۡنُ يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡمَلَأُ مَا عَلِمۡتُ لَكُم مِّنۡ إِلَٰهٍ غَيۡرِي فَأَوۡقِدۡ لِي يَٰهَٰمَٰنُ عَلَى ٱلطِّينِ فَٱجۡعَل لِّي صَرۡحٗا لَّعَلِّيٓ أَطَّلِعُ إِلَىٰٓ إِلَٰهِ مُوسَىٰ وَإِنِّي لَأَظُنُّهُۥ مِنَ ٱلۡكَٰذِبِينَ ٣٨
Waqāla fir'awnu yā'ayyuhal-mala'u mā 'alimtu lakum min ilāhin ghayrī fa awqid lī yāhāmānu 'alat-tīni faj'al lī sarhal la'allī attali'u ilā ilāhi mūsā wa innī la azunnuhū minal-kādhibīn
Na Firauni akasema: Enyi waheshimiwa! Sijui kama mnaye mungu asiye kuwa mimi. Ewe Haman! Niwashie moto unichomee udongo, unijengee mnara nipate kumchungulia mungu wa Musa. Na hakika mimi namwona yeye ni katika waongo. 38
Maelezo ya chini
38 Na Firauni alipo shindwa kuhojiana na Musa, na akaendelea na jeuri zake, alisema: Enyi wahishimiwa! Mimi sijui kama yupo mungu wenu mwenginewe isipo kuwa mimi. Na akamuamrisha waziri wake Haman amchomee matufali, na amjengee mnara mrefu apande, ende kumtazama huyo mungu anaye mlingania Musa.