قَالَ سَنَشُدُّ عَضُدَكَ بِأَخِيكَ وَنَجۡعَلُ لَكُمَا سُلۡطَٰنٗا فَلَا يَصِلُونَ إِلَيۡكُمَا بِـَٔايَٰتِنَآۚ أَنتُمَا وَمَنِ ٱتَّبَعَكُمَا ٱلۡغَٰلِبُونَ ٣٥
Qāla sanashuddu 'adudaka bi akhīka wanaj'alu lakumā sultānan falā yasilūna ilaykumā bi'āyātinā antumā wamanit-taba'akumal-ghālibūn
(Mwenyezi Mungu) akasema: Tutautia nguvu mkono wako kwa nduguyo, na tutakupeni madaraka, hata wasikufikilieni. Kwa sababu ya Ishara zetu nyinyi na watakao kufuateni mtashinda. 35
Maelezo ya chini
35 Mwenyezi Mungu akasema, kuitikia ombi lake: Tutakutia nguvu kwa kumtuma Harun. Na tutakupeni nyinyi wawili madaraka, na tutakuungeni mkono kwa miujiza. Kwa hivyo hawatoweza kukuvamieni. Na nyinyi wawili na walio kufuateni na wakaongoka kwa msaada wenu, mtakuwa wenye kuwashinda hawa makafiri.