Surat Al-Mu'minun, aya 33

23:33

وَقَالَ ٱلۡمَلَأُ مِن قَوۡمِهِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَكَذَّبُواْ بِلِقَآءِ ٱلۡأٓخِرَةِ وَأَتۡرَفۡنَٰهُمۡ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا مَا هَٰذَآ إِلَّا بَشَرٞ مِّثۡلُكُمۡ يَأۡكُلُ مِمَّا تَأۡكُلُونَ مِنۡهُ وَيَشۡرَبُ مِمَّا تَشۡرَبُونَ ٣٣

Waqālal-mala'u min qawmihil-ladhīna kafarū wakaddhabū biliqā'il-ākhirati wa atrafnāhum fil-hayawātid-dunyā mā hādhā illā basharum mithlukum ya'kulu mimmā ta'kulūna minhu wayashrabu mimmā tashrabūn

Na wakubwa katika watu wake walioukufuru, na wakakanusha mkutano wa Akhera, na tukawadekeza kwa starehe, katika maisha ya dunia, walisem: Huyu si chochote ila ni mwanadamu kama nyinyi, anakula mlacho, na anakunywa mnywacho. 33

Maelezo ya chini

33 Na wakubwa katika kaumu yake walio kufuru na kukadhibisha kukutana na Mwenyezi Mungu na mambo ya Akheria ya hisabu na malipo, na tukawapa sehemu kubwa ya starehe na neema, wakasema kwa kukanusha wito wake, na kuwazuia watu wasimfuate: Hapana khitilafu yo yote baina ya Huud na nyinyi. Anakula chakula hicho hicho mnacho kila nyinyi. Na anakunywa vinywaji hivyo hivyo mnavyo vinywa nyinyi. Mfano wa huyu hawezi kuwa Mtume, kwa sababu hana sifa msizo kuwa nazo nyinyi.