وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوۡمِهِۦ فَقَالَ يَٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَٰهٍ غَيۡرُهُۥٓۚ أَفَلَا تَتَّقُونَ ٢٣
Walaqad arsalnā nūhan ilā qawmihī faqāla yāqawmi'budullāha mā lakum min ilāhin ghayruhū afalā tattaqūn
Na hakika tulimtuma Nuhu kwa watu wake, akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna mungu asiye kuwa Yeye. Basi je! Hamwogopi? 23
Maelezo ya chini
23 Na katika visa vya watu wa kale pana mazingatio kwa ajili yenu mpate kuamini. Basi Sisi tulimtuma Nuhu kwa watu wake, naye akawaambia: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu pekee. Kwani nyinyi hamna anaye stahiki kuabudiwa asiye kuwa Yeye. Hamwogopi adhabu yake, na kuondoka neema zake mkimuasi?