أَلَمۡ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۖ مَا يَكُونُ مِن نَّجۡوَىٰ ثَلَٰثَةٍ إِلَّا هُوَ رَابِعُهُمۡ وَلَا خَمۡسَةٍ إِلَّا هُوَ سَادِسُهُمۡ وَلَآ أَدۡنَىٰ مِن ذَٰلِكَ وَلَآ أَكۡثَرَ إِلَّا هُوَ مَعَهُمۡ أَيۡنَ مَا كَانُواْۖ ثُمَّ يُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُواْ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۚ إِنَّ ٱللَّهَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٌ ٧
Alam tara annallāha ya'lamu mā fis-samāwāti wamā fil-ardi mā yakūnu min najwā thalāthatin illā huwa rābi'uhum walā khamsatin illā huwa sādisuhum walā adnā min dhālika walā akthara illā huwa ma'ahum ayna mā kānū thumma yunabbi'uhum bimā 'amilū yawmal-qiyāmati innallāha bikulli shay'in 'alīm
Kwani huoni kwamba Mwenyezi Mungu anajua vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi? Hauwi mnong'ono wa watu watatu ila Yeye huwa ni wane wao, wala wa watano ila Yeye huwa ni wa sita wao. Wala wa wachache kuliko hao, wala walio wengi zaidi, ila Yeye yu pamoja nao popote pale walipo. Kisha Siku ya Kiyama atawaambia waliyo yatenda. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu. 7
Maelezo ya chini
7 Kwani hujui kwamba Mwenyezi Mungu anayajua yaliomo mbinguni na yaliomo katika ardhi, na wala hapana siri ya watu watatu ila Yeye Mwenyezi Mungu ndiye wane wao kwa kuyajua kwake wanayo fanyia siri, wala hawawi watano ila na Yeye ndiye wa sita wao. Wala duni kuliko hivyo, wala kuzidi hivyo, ila Yeye yuko pamoja nao, anayajua hayo wanayo yanong'ona, popote walipo. Kisha Siku ya Kiyama atawapa khabari kwa kila walilo litenda. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kutimia ujuzi wake.