يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِذَا نَٰجَيۡتُمُ ٱلرَّسُولَ فَقَدِّمُواْ بَيۡنَ يَدَيۡ نَجۡوَىٰكُمۡ صَدَقَةٗۚ ذَٰلِكَ خَيۡرٞ لَّكُمۡ وَأَطۡهَرُۚ فَإِن لَّمۡ تَجِدُواْ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٌ ١٢
Yā'ayyuhal-ladhīna āmanū idhā nājaytumur-rasūla faqaddimū bayna yaday najwākum sadaqatan dhālika khayrul lakum wa atharu fa il lam tajidū fa innallāha ghafūrur rahīm
Enyi mlio amini! Mnapo sema siri na Mtume, basi tangulizeni sadaka kabla ya kusemezana kwenu. Hiyo ni kheri kwenu na usafi zaidi. Na ikiwa hamkupata cha kutoa, basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. 12
Maelezo ya chini
12 Enyi mlio msadiki Mwenyezi Mungu na Mtume wake! Mkitaka kusema siri na Mtume wa Mwenyezi Mungu, basi kabla ya mazungumzo yenu hayo tangulizeni kutoa sadaka. Hivyo ndio kheri yenu, na ni usafi zaidi kwa nyoyo zenu. Lakini ikiwa hamkupata cha kutoa sadaka, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu wa kusamehe, Mwenye kukusanya rehema zote.