فَمَنِ ٱبۡتَغَىٰ وَرَآءَ ذَٰلِكَ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡعَادُونَ ٣١
Famanibtaghā warā'a dhālika fa ulā'ika humul-'ādūn
Lakini wanao taka kinyume ya haya, basi hao ndio wanao ruka mipaka. 31
Maelezo ya chini
31 Basi mwenye kutafuta starehe ya maingiliano kwa wasio kuwa wake na masuria, basi hao tena ni wenye kuikiuka halali na kuingia katika haramu.