Surat Al-Kahf, aya 54

18:54

وَلَقَدۡ صَرَّفۡنَا فِي هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانِ لِلنَّاسِ مِن كُلِّ مَثَلٖۚ وَكَانَ ٱلۡإِنسَٰنُ أَكۡثَرَ شَيۡءٖ جَدَلٗا ٥٤

Walaqad sarrafnā fī hādhal-qur'āni lin-nāsi min kulli mathalin wakānal-insānu akthara shay'in jadalā

Na bila ya shaka tumewaelezea watu katika hii Qur'ani kila namna ya mfano. Lakini mwanaadamu amezidi kuliko kila kitu kwa ubishi. 54

Maelezo ya chini

54 Na Mwenyezi Mungu amewatajia watu katika Qur'ani hii, wanayo ikanusha na wakataka waletewe muujiza mwenginewe, mifano namna kwa namna, ili wapate kuwaidhika kwayo. Lakini mwanaadamu tabia yake ni kupenda kubishana. Akiwa kafiri basi atabisha hata kwa uwongo.